Wachangiaji wa Wikipedia ya Kiswahili

Hivi una habari kama zamani kulikuwa na Mswahili mmoja tu kwenye Wikipedia ya Kiswahili? Mswahili huyo ni Ndesanjo. Ndesajo, alichangia Wikipedia ya Kiswahili akiwa na rundo la Wazungu – kiasi kwamba alihisi hata upweke. Kilichotokea? Hatujui, lakini amekimbia jumla tena. Vilevile kuliwa na Joel Niganile kutoka Tanga. Mara ya mwisho kuhairi ilikuwa tarehe 17 Novemba, 2007, wakati Ndesanjo mara ya mwisho kuhariri ilikuwa tarehe 30 Agosti 2017 – huwa anaingia na kutoka na si mchangiaji wa moja kwa moja kama zamani. Wapo waliokuwepo pia waja na kutoka au kuweko kwa muda mrefu halafu wamepotea moja kwa moja, mfano: Msafiri. Kijana aliyeakuwa anasoma huko Misri, lakini ana asili ya Burundi. Kijana ambaye alionesha mapenzi juu ya uandishi wa makala za mpira. Mara ya mwisho kuchangia, Januari 11 2012. Wengi wao ni Wazungu walewale waliobaki: Kipala, Baba Tabita na Riccardo Riccioni.

Categories:

Leave a comment