Gangwe Mobb – Wikipedia

GWM na Gangwe Mob
Kushoto, Inspector Haroun na Dogo Side, kulia Di-Chief na KR Mullah.

Gangwe Mobb ni kundi la muziki wa hip hop ya Kitanzania. Kundi linatokea katika maeneo ya Temeke Mikoroshini huko mjini Dar es Salaam. Kundi linaunganishwa na wanachama wawili ambao ni: Inspector Haroun (jina kamili ni Haroun Kahena) na Luteni Karama (Karama Bakari). Kundi hili lilianzishwa mwishoni mwa miaka ya 90 punde baada ya Kwanza Unit, Mr. II na wengineo waliosababisha muziki wa hip hop wa Kiswahili nchini Tanzania kujipatia umaarufu. Jina la “Gangwe” linatokana na istilahi ya neno la msimu mashuhuri la Kiingereza la miaka ya 80 “hardcore”. Ki-muktadha, gangwe inalenga hasa uhalisia wa hip hop ya watu wa mtaani ambamo mara nyingi wanaimba kwenye nyimbo zao. [1]

Kibao chao cha kwanza mashuhuri kilikuwa “Mauzauza”. Albamu yao ya kwanza, “Simulizi la Ufasaha” ikiwa imejumlisha vibao vikali ambavyo ni “Ngangali” na “Mtoto wa Geti Kali”. Albamu yao ya pili ni “Nje Ndani”, ilitolewa mnamo mwaka wa 2002 ilikuwa na kibao chake kilicholeta gumzo, “Asali wa Moyo”. Miongoni mwa single zao walipata kuziita “Bundasiliga” ambazo zilikuwa zikitoa ujumbe kwa jamii. [2] Pia wamewahi kushirikiana na kundi la Kikenya la Necessary Noize kwenye kibao cha “Tunajirusha”.

Gangwe Mobb wanaeleza kwamba muziki wao kama rap katuni. Inaelezea kuhusu hali halisi ya maisha ya watu hali chini jinsi wanavyo-haha katika kujitafutia riziki ya kila siku. Nyimbo zao pia zinajulikana kwa kuanzisha lahaja mpya ya maneno ya msimu kwa kila nyimbo yao. Mengi tazama Wikipedia.

Advertisements
Categories:

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s