Tamasha la Mwaka 2000 – Wikipedia

Mwaka Elfu Mbili lilikuwa jina lililotolewa kwa ajili ya tamasha lililofanyika mnamo DarEventAHH tangazotarehe 9 Mei, 1999 huko jijini Dar es Salaam, Tanzania. Tamasha hili liliandaliwa na Madunia Foundation na kudhaminiwa na Salama Condoms na msaada wa taarifa zinazopatikana katika wavuti ya Rumba Kali wakati huo (sasa African Hip Hop.com). Dhumuni la kufanya onesho hili ilikuwa kuanda vipande vya filamu kwa ajili ya dokumentari ya “Hali Halisi. [1] Tamasha lilifanyika katika ukumbi wa FM Club Kinondoni.

Wazo kuu linatoka kwa Martin Meulenberg (ambaye ndiye aliyeongoza utengenezwaji wa filamu ya Hali Halisi) na ndiye aliyependekeza kuandaa onesho hili kwa nia ya kukusanya maoni mbalimbali kutoka kwa wasanii tofauti. Kwa kutumia taarifa zilizokusanywa na mtandao wa Rumba Kali, ilikuwa rahisi kutengeneza vipepereshi vinavyotoa taarifa kuhusu onesho hili. Wakati wa onesho walifanikiwa kufanya mahojiano na wasanii zaidi ya ishirini kisha baadaye wakaenda Arusha na Zanzibar.

Mengi kuhusu tamasha la Mwaka 2000 tazama hapa katika Wikipedia ya Kiswahili.

Gangwe Mobb upande wa kushoto (Inspector Haroun kainamia meza anaandika) na wa mbele yake Dogo Side, na G.W.M. upande wa kulia (D-Chief kushoto na KR Mullah kulia).

Baadhi ya wasanii walionekana kwenye posta ya tamasha hili ni pamoja na Gangwe Mobb, Deplowmatz, G.W.M, Unique Sisters, II Proud, KBC (Kwanza Unit, Underground Souls, Xplastaz, Fortune Tellers na wasanii wengine ambao walitangazwa katika redio ya Clouds kipindi ndiyo inaanzishwa. Wakati huu KBC alikuwa mtangazaji katika kipindi cha kila wiki cha “Underground hip hop Show.

Advertisements
Categories:

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s